Namshukuru Mungu kwa siku ya leo maana Bila yeye nisingeweza kufanya hiki yote ni kwa utukufu wake.
Kuna wakati unakuwa unamwitaji mtu ambaye unahisi anaweza kutimiza ndoto yako ya kuwa na familia bora yenye Amani na upendo.
Na unatumia pesa na nguvu ulizo nazo Bila kumdhirikisha Mungu, inataka dakika ya mwisho unaona hakufai.
Mungu ni mwaminifu sana Kwa watu wake na ametuaihidi mambo Mengi mazuri ikiwemo mke mwema na Mume mwenye hekima.
Embu Anza sasa kuzungumza na Mungu katika moyo wako ukimuuliza na kumwelezea kile unachokitaka na ikiwezekana andaa moyo wako kwa ajili ya furaha na mtu mpya.
Mungu hajawahi kushindwa hata siku moja, binadamu tunashindwa na kupata tamaa ila msaada uko wa Mungu aliye hai.
Mimi nina ushuhuda wa kweli kabisa Mungu alinitendea wakati namwomba anipe Mume kulikuwa na vikwanzo vingi ila mwisho akaniinua maadui wakaa pembeni.
Hata wewe unayesoma makala hii Inawezekana Kuna mtu anausumbua moyo wako na umefika mahali unaona uwezi tena kuendelea naye mwambie Mungu.
Kwa kutembelea mahabati utajifunza Mengi sana usichoke Soma maana maarifa Mengi yapo hapa mahabati.
Kumbuka kuwa Mungu ni Mungu tu haijalishi wanakuta jina gani wewe ni mshindi katika ndoa yako na mahusiano yako.
Usiache kutoa maoni yako jinsi ulivyosaidika na mahabati
No comments:
Post a Comment