KARIBU TENA

KARIBU TENA

Sunday, June 19, 2016

Mapenzi kikohonzi kuyaficha siwezi

Nashukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau wa blog ya mapreciouswaukweli.blogspot.com kwa kuendelea kutembelea na kupata maujuzi zaidi ya mahusiano.

Ama kweli mapenzi kikohonzi kuyaficha si rahis, ninachokizungumza kila mlenga kila mmoja wetu Bila kuangalia umri.

Siku moja nilikuwa natembea nikakutana na kuku jogoo na mtetea wanabembelezana nikasisimka nikawaangalia kisha nikasema kweli mapenzi kikohonzi.

Kila kiumbe chenye uhai kinamapenzi sasa kwa binadamu ndiyo inanishangaza zaidi wadau wangu.

Kila siku  napokea ujumbe humu ndani ndani, Kuna mdau yeye anapenda sana mkewe ila mkewe haioni wala hajali anaumia sana kwa sababu Kuna wakati anashindwa hata kufanya kazi zake vizuri.

Siku moja mdau mwingine naye anasema mume wake ni kidonda kila siku lazima amuumize moyo wake, na huyo mrembo anampenda mpaka halali usingizi wake amehamishia kwa jamaa.

Haya mapenzi kweli kikohonzi kuyaficha hatari jamani unapogundua kuwa unapendwa acha kuchezea moyo wa mwezako maana ipo siku inakuja utajuta. 

Mapenzi si kitu cha kujaribu maana yana madhara makubwa ya kisaikolojia na kimwili wengi wameshindwa hata kufanya kazi na majukumu yao mengine.   

Sasa wewe unasikia raha gani kuishi ukiwa unanig'iniza moyo wa mwezako hewani Muda wote?

Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwingine kumbuka dunia Mapito tupo safarini hapa hakuna aliyenitakia.

Kumbukumbu kumtanguliza Mungu kwa kila jambo maana njia zake hazichunguziki yeye anatibu maumivu uliyo nayo .

Endelea kutembelea mahabati uelimike zaidi mapreciouswaukweli.blogspot.com huku Kuna makala motomoto za mahaba.

No comments:

Post a Comment