KARIBU TENA

KARIBU TENA

Sunday, June 19, 2016

Akina baba wapendeni watoto wenu Bila kujali jinsia

Katika kusherekea siku ya baba duniani akina baba embu tumieni siku yenu hii kudumisha upendo wenu kwa familia na hususani watoto.

Nimeamua kuandika makala hii nikijua wazi kuwa Kuna akina baba wengi wamejenga chuki kwa watoto wao kisa ni wa jinsia fulani.

Baba unajisahau kuwa wewe ndiyo uliyepanda mbegu hizo au unadhani mayai yanaweza kujibadilisha na kuwa jinsi fulani? 

Hili limekuwa tatizo kwa wanandoa wengi na baadhi ya Ndugu wa mwanaume kuwa mkeo hazai watoto wa kike anazaa wa kiume tu.

Baba umesahau kuwa yule rafiki yako hana hata mmoja na anaomba usiku na mchana apate wa jinsia yoyote.

Wewe baba usimpangie Mungu yeye Ndiye anayepanga kukupa,  sasa mbona unalalama sana.

Akina baba jitahidini kuridhika na hali halisi na ikiwezekana shirikiana na mwezako kujenga familia bora na Mungu atawabariki.

Nawatakia Akina baba wote sikuku njema msherehekee kwa Amani na upendo katika familia zetu kumbuka kuteleza siyo kuanguka happy Father's day.

Nawapenda sana wazazi wangu na watoto wangu Mungu awabariki.

No comments:

Post a Comment