KARIBU TENA

KARIBU TENA

Monday, June 27, 2016

Mleye mtoto katika njia impasayo naye ataiacha hata uzeeni

Nashukuru Mungu kwa utukufu wake maana ni wengi walitamani kufika Muda huu lakini hajafika.

Wengine ni watoto wadogo, vijana na wazee tuliyowategemea kutupa ushauri katika masuala mbalimbali lakini Mungu amewapenda zaidi.

Inawezekana ni mama mjamzito amepoteza mtoto wake baada ya kujifungua yote tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa kazi yake haina makosa.

Kutokana na ugumu wa maisha baadhi ya wazazi wamejikuta wakishindwa kutimiza wajibu wao kwa watoto wao na kuwaachia watu wengine au kwa lugha nyingine walimwengu.

Mtoto wa mwezio ni mwanao siyo wote wanaozingatia kauli hii na kuifanyia kazi, wengine huitumia kinyume.

Najua wewe mama na baba uko busy kuwatafutia watoto wako maisha bora Anza sasa kutenga Muda wa kukaa na kumsikiliza mwanao, nini anataka nini hataki amekutana na shida gani kisha msaidie kwa kumpa njia sahihi ya kupita ili kutimiza ndoto yake.

Kwa kufanya hivi unajua Mengi anayokutana nayo, Mimi hapendi kumwambia mwanangu usimtendee mwezako ubaya maana Mungu hapendi, wengi wanaotenda mabaya ni watoto wa shetani.

Nimekuwa nikimfundisha mambo kadhaa na kuruhusu kuniuliza maswali kadhaa na la msingi husisitiza kushirikishana Mungu katika kila jambo analota kulifanya maishani mwake. 

Huu ni msingi mzuri naamini hata wewe ukifanya hivyo utakuwa na watoto wema wacha Mungu.

Nakushukuru wewe mzazi mwema unapitia makala hii ubarikiwe sana na Mungu akulindie watoto wako, kumbuka watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu itunze na kuipenda.

Thursday, June 23, 2016

Nakupongeza sana mwanazuoni mwezangu Grace Kihampa

Napenda kutumia Muda huu kumpongeza mwanahabari na kipenzi cha wengi Grace Kihampa kwa kutimiza miaka kadhaa leo.

Mungu akubariki akulinde na kukufikisha mbali zaidi katika tasnia hii ya habari hakika unastahili pongezi.

Usimuliaji wako wa habari ni mfano wa kuigwa na wanahabari waliyo wengi hapa nchini wenye kupenda kujifunza.

Mungu aendelee kukung'arisha katika tasnia hii ya habari mpendwa wangu, kumbuka kumshukuru Mungu kwa kila jambo....

Mshukuru Mungu kwa kila jambo

Namshukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau wa blog ya mapreciouswaukweli.blogspot.com nakupenda sana.

Wewe ni mdau wangu wa nguvu kutendo cha kutumia Muda wako kutembelea blog hii ni upendo wa pekee.

Napenda kutumia Muda huu kukushukuru na kumshukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau.

Namshukuru Mungu kwa kuwa hai mpaka leo hii na kunipa hekima ya kutumia mtandao kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali.

Naimani na wewe una Mengi ya kumshukuru Mungu kwa ajili yako tumia Muda huu kurudishia mungu sifa na utukufu.

Kutendo cha kukupa mtu unayempenda na manaishi kwa furaha unapaswa kumshukuru kwa Hilo.

Tuesday, June 21, 2016

Kupendeza kwa mwenza wako hakuna umri wala cheo

Namshukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau wangu wa nguvu, unaendelea kutembelea blog yangu  ya mapreciouswaukweli.blogspot.com na kujifunza mambo Mengi ya kujenga familia bora na mahusiano kwa ujumla.

Hakika katika maisha ya kawaida kila mtu anapenda kumtanzama mtu aliye pendeza tena mwingine humsindikiza kwa macho hadi anapoishia wengine huanza safari ya kumfatilia mtu huyo hadi mwisho.

Usishangae Inawezekana wewe ujawahi kukutana na kasumba hiyo ila tembea uone Mengi.

Wahenga walisema kua uyaone siyo majengo hapana Kuna watu wanajipenda chini yajua ukiwaona unaweza ukadhani malaika.

Suala la kujipenda wengine ni hulka lakini siyo hulka mbaya ni nzuri hata wewe unaweza kwanza kuitumia ili kujenga familia bora yenye afya inayojipenda.
 
Mtu anayejipenda hawezi kufanya ngono ovyo wala na mtu asiyemjua vizuri, hivyo unadhifu huo utakuepusha na Mengi yakiwemo maradhi ya zinaa na Ukimwi. 

Hii siyo kwa wanawake tu hata wanaume wanapaswa kujifunza kwa kuanzia mwilini mwao, mavazi hadi katika malazi.

Inawezekana unakimbiwa mtu unaye fikiria anaweza kuwa mke au mme kila siku wewe unalia kwenye mapenzi unajiuliza Pengine wewe hujui kupenda nini kumbe tatizo ni hulka yako ya uchafu.

Nguo zenyewe unavaa ilimradi tu umevaa alafu unajiuliza kwanini wewe hausifiwi kama wengine kuwa umependeza?  Badilika usivae nguo za aina moja.

Tatizo siyo sura tatizo mwonekano wako hauridhishi na jasho nalo unanuka embu nusu kwapa lako, unalisikiaje vipi kwa mtu mwingine anaweza kustahimili.

Kujipenda hakuchagui umri wala cheo umaridadi uficha umasikini jipende kabla ya kupendwa na mtu mwingine.

Kwa leo naomba niishie hapa nawapongeza wale wote ambao umri umeenda na bado wanajipenda.

Endelea kutembelea mapreciouswaukweli.blogspot.com kwa ubunifu zaidi,uokoe familia yako na nyumba yako kwa ujumla.

Sunday, June 19, 2016

Akina baba wapendeni watoto wenu Bila kujali jinsia

Katika kusherekea siku ya baba duniani akina baba embu tumieni siku yenu hii kudumisha upendo wenu kwa familia na hususani watoto.

Nimeamua kuandika makala hii nikijua wazi kuwa Kuna akina baba wengi wamejenga chuki kwa watoto wao kisa ni wa jinsia fulani.

Baba unajisahau kuwa wewe ndiyo uliyepanda mbegu hizo au unadhani mayai yanaweza kujibadilisha na kuwa jinsi fulani? 

Hili limekuwa tatizo kwa wanandoa wengi na baadhi ya Ndugu wa mwanaume kuwa mkeo hazai watoto wa kike anazaa wa kiume tu.

Baba umesahau kuwa yule rafiki yako hana hata mmoja na anaomba usiku na mchana apate wa jinsia yoyote.

Wewe baba usimpangie Mungu yeye Ndiye anayepanga kukupa,  sasa mbona unalalama sana.

Akina baba jitahidini kuridhika na hali halisi na ikiwezekana shirikiana na mwezako kujenga familia bora na Mungu atawabariki.

Nawatakia Akina baba wote sikuku njema msherehekee kwa Amani na upendo katika familia zetu kumbuka kuteleza siyo kuanguka happy Father's day.

Nawapenda sana wazazi wangu na watoto wangu Mungu awabariki.

Mapenzi kikohonzi kuyaficha siwezi

Nashukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau wa blog ya mapreciouswaukweli.blogspot.com kwa kuendelea kutembelea na kupata maujuzi zaidi ya mahusiano.

Ama kweli mapenzi kikohonzi kuyaficha si rahis, ninachokizungumza kila mlenga kila mmoja wetu Bila kuangalia umri.

Siku moja nilikuwa natembea nikakutana na kuku jogoo na mtetea wanabembelezana nikasisimka nikawaangalia kisha nikasema kweli mapenzi kikohonzi.

Kila kiumbe chenye uhai kinamapenzi sasa kwa binadamu ndiyo inanishangaza zaidi wadau wangu.

Kila siku  napokea ujumbe humu ndani ndani, Kuna mdau yeye anapenda sana mkewe ila mkewe haioni wala hajali anaumia sana kwa sababu Kuna wakati anashindwa hata kufanya kazi zake vizuri.

Siku moja mdau mwingine naye anasema mume wake ni kidonda kila siku lazima amuumize moyo wake, na huyo mrembo anampenda mpaka halali usingizi wake amehamishia kwa jamaa.

Haya mapenzi kweli kikohonzi kuyaficha hatari jamani unapogundua kuwa unapendwa acha kuchezea moyo wa mwezako maana ipo siku inakuja utajuta. 

Mapenzi si kitu cha kujaribu maana yana madhara makubwa ya kisaikolojia na kimwili wengi wameshindwa hata kufanya kazi na majukumu yao mengine.   

Sasa wewe unasikia raha gani kuishi ukiwa unanig'iniza moyo wa mwezako hewani Muda wote?

Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwingine kumbuka dunia Mapito tupo safarini hapa hakuna aliyenitakia.

Kumbukumbu kumtanguliza Mungu kwa kila jambo maana njia zake hazichunguziki yeye anatibu maumivu uliyo nayo .

Endelea kutembelea mahabati uelimike zaidi mapreciouswaukweli.blogspot.com huku Kuna makala motomoto za mahaba.

Saturday, June 18, 2016

Usikate tamaa kwa kuchelewa kuoa au kuolewa

Namshukuru Mungu kwa ajili yako wewe unayesoma makala hii jiandae kupata kitu kipya katika maisha yako.

Kuchelewa kuolewa au kuoa kwa waliyo wengi imekuwa ni moja ya changamoto inayowasumbua wengi kimwili na kisaikolojia.

Wengi wamejikuta wakikata tamaa na kuchukua maamuzi ambayo haujibu mfumo mzima wa maisha.

Wengine wajikuta wanazaa na waume za watu na kusababisha watoto kukosa malenzi bora na kujizolea lana.

Siku moja nilikutana na mdau wangu ananiambia anajutia maisha yake kwa kuzaa na Mume wa mtu sasa mtoto anamsumbua anamtaka baba yake na huyo mwanaume hataki hata kusikia.

Inaumiza sana wengine hujikuta wanaangukia kwa mashuga mamy au wazee wanaolingana na wazee wao.

Kila jambo lina wakati wake kama uliteleza mwombe Mungu akuumbe upya mwombe Mungu toba ya kweli akutengeneze upya uanze maisha mapya.

Mume wako yuko anakuja endelea kusubiria ukiwa katika maombi Mungu hachelewi wala Hawai.

Mungu amekupangia mambo Mengi mazuri amini hivyo na ipo siku utasema kupitia blog hii....

Tuesday, June 14, 2016

Bila Mungu uwezi kufaulu kumpata huyo

Namshukuru Mungu kwa siku ya leo maana Bila yeye nisingeweza kufanya hiki yote ni kwa utukufu wake.

Kuna wakati unakuwa unamwitaji mtu ambaye unahisi anaweza kutimiza ndoto yako ya kuwa na familia bora yenye Amani na upendo.

Na unatumia pesa na nguvu ulizo nazo Bila kumdhirikisha Mungu, inataka dakika ya mwisho unaona hakufai.

Mungu ni mwaminifu sana Kwa watu wake na ametuaihidi mambo Mengi mazuri ikiwemo mke mwema na Mume mwenye hekima.

Embu Anza sasa kuzungumza na Mungu katika moyo wako ukimuuliza na kumwelezea kile unachokitaka na ikiwezekana andaa moyo wako kwa ajili ya furaha na mtu mpya.

Mungu hajawahi kushindwa hata siku moja, binadamu tunashindwa na kupata tamaa ila msaada uko wa Mungu aliye hai.

Mimi nina ushuhuda wa kweli kabisa Mungu alinitendea wakati namwomba anipe Mume kulikuwa na vikwanzo vingi ila mwisho akaniinua maadui wakaa pembeni.

Hata wewe unayesoma makala hii Inawezekana Kuna mtu anausumbua moyo wako na umefika mahali unaona uwezi tena kuendelea naye mwambie Mungu.

Kwa kutembelea mahabati utajifunza Mengi sana usichoke Soma maana maarifa Mengi yapo hapa mahabati.

Kumbuka kuwa Mungu ni Mungu tu haijalishi wanakuta jina gani wewe ni mshindi katika ndoa yako na mahusiano yako. 

Usiache kutoa maoni yako jinsi ulivyosaidika na mahabati