KARIBU TENA

KARIBU TENA

Saturday, June 18, 2016

Usikate tamaa kwa kuchelewa kuoa au kuolewa

Namshukuru Mungu kwa ajili yako wewe unayesoma makala hii jiandae kupata kitu kipya katika maisha yako.

Kuchelewa kuolewa au kuoa kwa waliyo wengi imekuwa ni moja ya changamoto inayowasumbua wengi kimwili na kisaikolojia.

Wengi wamejikuta wakikata tamaa na kuchukua maamuzi ambayo haujibu mfumo mzima wa maisha.

Wengine wajikuta wanazaa na waume za watu na kusababisha watoto kukosa malenzi bora na kujizolea lana.

Siku moja nilikutana na mdau wangu ananiambia anajutia maisha yake kwa kuzaa na Mume wa mtu sasa mtoto anamsumbua anamtaka baba yake na huyo mwanaume hataki hata kusikia.

Inaumiza sana wengine hujikuta wanaangukia kwa mashuga mamy au wazee wanaolingana na wazee wao.

Kila jambo lina wakati wake kama uliteleza mwombe Mungu akuumbe upya mwombe Mungu toba ya kweli akutengeneze upya uanze maisha mapya.

Mume wako yuko anakuja endelea kusubiria ukiwa katika maombi Mungu hachelewi wala Hawai.

Mungu amekupangia mambo Mengi mazuri amini hivyo na ipo siku utasema kupitia blog hii....

No comments:

Post a Comment