KARIBU TENA

KARIBU TENA

Monday, June 27, 2016

Mleye mtoto katika njia impasayo naye ataiacha hata uzeeni

Nashukuru Mungu kwa utukufu wake maana ni wengi walitamani kufika Muda huu lakini hajafika.

Wengine ni watoto wadogo, vijana na wazee tuliyowategemea kutupa ushauri katika masuala mbalimbali lakini Mungu amewapenda zaidi.

Inawezekana ni mama mjamzito amepoteza mtoto wake baada ya kujifungua yote tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kuwa kazi yake haina makosa.

Kutokana na ugumu wa maisha baadhi ya wazazi wamejikuta wakishindwa kutimiza wajibu wao kwa watoto wao na kuwaachia watu wengine au kwa lugha nyingine walimwengu.

Mtoto wa mwezio ni mwanao siyo wote wanaozingatia kauli hii na kuifanyia kazi, wengine huitumia kinyume.

Najua wewe mama na baba uko busy kuwatafutia watoto wako maisha bora Anza sasa kutenga Muda wa kukaa na kumsikiliza mwanao, nini anataka nini hataki amekutana na shida gani kisha msaidie kwa kumpa njia sahihi ya kupita ili kutimiza ndoto yake.

Kwa kufanya hivi unajua Mengi anayokutana nayo, Mimi hapendi kumwambia mwanangu usimtendee mwezako ubaya maana Mungu hapendi, wengi wanaotenda mabaya ni watoto wa shetani.

Nimekuwa nikimfundisha mambo kadhaa na kuruhusu kuniuliza maswali kadhaa na la msingi husisitiza kushirikishana Mungu katika kila jambo analota kulifanya maishani mwake. 

Huu ni msingi mzuri naamini hata wewe ukifanya hivyo utakuwa na watoto wema wacha Mungu.

Nakushukuru wewe mzazi mwema unapitia makala hii ubarikiwe sana na Mungu akulindie watoto wako, kumbuka watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu itunze na kuipenda.

No comments:

Post a Comment