KARIBU TENA

KARIBU TENA

Tuesday, June 21, 2016

Kupendeza kwa mwenza wako hakuna umri wala cheo

Namshukuru Mungu kwa ajili yako wewe mdau wangu wa nguvu, unaendelea kutembelea blog yangu  ya mapreciouswaukweli.blogspot.com na kujifunza mambo Mengi ya kujenga familia bora na mahusiano kwa ujumla.

Hakika katika maisha ya kawaida kila mtu anapenda kumtanzama mtu aliye pendeza tena mwingine humsindikiza kwa macho hadi anapoishia wengine huanza safari ya kumfatilia mtu huyo hadi mwisho.

Usishangae Inawezekana wewe ujawahi kukutana na kasumba hiyo ila tembea uone Mengi.

Wahenga walisema kua uyaone siyo majengo hapana Kuna watu wanajipenda chini yajua ukiwaona unaweza ukadhani malaika.

Suala la kujipenda wengine ni hulka lakini siyo hulka mbaya ni nzuri hata wewe unaweza kwanza kuitumia ili kujenga familia bora yenye afya inayojipenda.
 
Mtu anayejipenda hawezi kufanya ngono ovyo wala na mtu asiyemjua vizuri, hivyo unadhifu huo utakuepusha na Mengi yakiwemo maradhi ya zinaa na Ukimwi. 

Hii siyo kwa wanawake tu hata wanaume wanapaswa kujifunza kwa kuanzia mwilini mwao, mavazi hadi katika malazi.

Inawezekana unakimbiwa mtu unaye fikiria anaweza kuwa mke au mme kila siku wewe unalia kwenye mapenzi unajiuliza Pengine wewe hujui kupenda nini kumbe tatizo ni hulka yako ya uchafu.

Nguo zenyewe unavaa ilimradi tu umevaa alafu unajiuliza kwanini wewe hausifiwi kama wengine kuwa umependeza?  Badilika usivae nguo za aina moja.

Tatizo siyo sura tatizo mwonekano wako hauridhishi na jasho nalo unanuka embu nusu kwapa lako, unalisikiaje vipi kwa mtu mwingine anaweza kustahimili.

Kujipenda hakuchagui umri wala cheo umaridadi uficha umasikini jipende kabla ya kupendwa na mtu mwingine.

Kwa leo naomba niishie hapa nawapongeza wale wote ambao umri umeenda na bado wanajipenda.

Endelea kutembelea mapreciouswaukweli.blogspot.com kwa ubunifu zaidi,uokoe familia yako na nyumba yako kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment