KARIBU TENA

KARIBU TENA

Sunday, October 13, 2013

Bonnah Education Trust Fund ikidhaminiwa na kampuni ya Simu ya mkonon Tigo yafanya uzinduzi wa mfuko wa elimu wa aina yake.


Mkurugenzi wa Bonnah Education Trust fund Bi Bonnah Kaluwa  aelezea kufurahishwa na mafanikio ya uzinduzi wa mfuko wa kusaidia watoto wasiyokuwa na uwezo wa kulipa ada waliyofaulu kuingia kidato cha kwanza iliyofadhiliwa na Kampuni ya simu ya mkononi ya nchini Tanzania Tigo


Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya mavazi wakiwa jukwani na ujumbe wa elimu kwa jamii kama unavyoonekana katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi mtendaji wa Bonnah Education Trust Fund Katikati akiwa na washiriki wa maonyesho ya mavazi jana mlin City jijini Dar es salaam

Mkurugenzi Bonnah Akiwa na Vijana wa maonyesho ya sarakasi waliyokuwa wakinogesha uzinduzi wa mfuko huo wa kuhamasisha kuchangia elimu.


Kushoto ni Bi Regina Ogwao katikati ni mkurugenzi wa Bonnah Education Trust Fund Bonnah Kaluwa nakulia ni Mwenyeki wa umoja wa vijana wa CCM Kata ya Kipawa Saidi Mkuwa Mlimani City Jijini Dar es salaam.


baadhi ya wadau wa Bonna Education Trust Fund wakijadiliana Jambo na mkurugenzi wa Bonnah Kaluwa

Akizungumza na Bloga hii mkurugenzi mtendaji wa Bonnah Education Trust Fund, na Diwani wa kata ya Kipawa jijini Dar Es salaam Mheshimiwa Bonnah Kaluwa alisema kuwa, uzinduzi huo umeambatana na maonyesho ya mavazi yaliyoanzia mnazi mmoja hadi mlimani City jijini Dar es Salaam.


Uzinduzi huo ulipambwa michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi, maonyesho ya mavazi, pamoja na mabango mbalimbali yaliyokuwa na ujumbe wa elimu.

Washiriki katika maonyesho hayo wameelezea kufurahishwa kwao na kitendo cha Mheshimiwa Bonnah Kaluwa,kutambua umuhimu wa elimu katika familia masikini na kuamua kuwasaidia.

Thursday, October 10, 2013

Mkurugenzi wa Bonnah Education Trust Fund amewataka watanzania kujenga utamaduni wa kusaidwatoto waliyofaulu darasa la saba na kukosa ada ya elimu ya sekondari kuendelea



Mkurugenzi wa Bonnah Education Trust Fund na Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam Mheshimiwa Bonnah Kaluwa ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupenda kusaidia watoto wanaofaulu elimu ya msingi ili kuendelea na elimu ya sekondari.
Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akizungumzia umuhimu wa elimu katika jamii namna ya kuwaendeleza watoto wenye uwezo wa kuelewa darasani

Mkurugenzi wa Bonnah Education Trust Fund na Diwani wa Kata ya Kipawa Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam Mheshimiwa Bonnah Kaluwa ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kupenda kusaidia watoto wanaofaulu elimu ya msingi ili kuendelea na elimu ya sekondari.


Mheshimiwa Kaluwa alisema idadi kubwa ya watoto wanaofanya vizuri wanatokea katika familia masikini, ambazo hazina uwezo wa kuwalipia ada watoto hao, hali inayowakwamisha watoto hao katika elimu ya sekodnari.


Alisema hayo wakati akifanya mahojiano maalumu na Blog ya mahabati katika hotel ya Serena iliyopo Posta jijini Dar es salaam.




Mheshimiwa Bonnah Kaluwa akihojiwa na mwasisi wa blog ya Mahabati Upendo Martin Mwase
 Aidha alisema moja ya changamto kubwa iliyopo katika elimu, ni uwezo mdogo wa baadhi ya familia ambazo watoto wanaofaulu wanatokea.


“mimi naumia sana kuona watoto wenye uwezo mkubwa wa elimu wakiwa wanashindwa kuendelea na elimu kwa sababu ya kukosa ada ambayo ni elfu 40 tu kwa mwaka, na ndiyo maana nimeamua sasa kuanzisha mfuko wa kuwasaidia watoto hao.

“kwa kuanza nimeanza na watoto mia moja ingawa watoto wako wengi ila mimi nimeamua nianze na hao, nimejaribu kuomba ufadhili katika kampuni zaidi ya 90, kamupuni 40 zimeonyesha moyo wa kunisaidia katika jitihada zangu hizi.

“kampuni ya simu za mikononi Tanzania Tigo imekubali kuwasomesha watoto zaidi ya 40, na mimi mwenyewe nasomesha watoto wengine watano kwa kushirikiana na Rafiki zangu”alisema Mheshimiwa Bonnah Kaluwa.

Hata hivyo aliongeza kuwa tatizo hilo ni la nchi nzima, ila kwa kuwanza yeye ameamua kuanza kwa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam.

Pamoja na mambo mengine aliwataka wanawake kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleao ili kujikwamua na umaskini.

Mheshimiwa Kaluwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Radio Mlimani, juu ya changamoto zinazowakabili wanawake.

Amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali wanawake wanapaswa kujiamini, na kwamba wanawake wanaweza kufikia asilimia 50 katika uongozi endapo watajiamini katika nafasi mablimbali wanazopewa kwenye jamii.

Tuesday, June 25, 2013

send off Part ya aina yeke terrat


Binti Lovenness Lomayani akiwa amesimama kwa ajili ya kukabidhiwa kwa baba wa kijana


Monday, June 24, 2013

SEND OFF PART YA LOVENNES LOMAYAN ILIYOFUNIKA ZAIDI YA ZA MJINI

Lovenness Lomayan akiwa na patna wake katika meza kuu siku ya send off part yake iliyofanyika nyumbani kwao terrat.