| Baadhi ya washiriki wa maonyesho ya mavazi wakiwa jukwani na ujumbe wa elimu kwa jamii kama unavyoonekana katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam. |
| Mkurugenzi mtendaji wa Bonnah Education Trust Fund Katikati akiwa na washiriki wa maonyesho ya mavazi jana mlin City jijini Dar es salaam |
Mkurugenzi Bonnah Akiwa na Vijana wa maonyesho ya sarakasi waliyokuwa wakinogesha uzinduzi wa mfuko huo wa kuhamasisha kuchangia elimu.
|
| baadhi ya wadau wa Bonna Education Trust Fund wakijadiliana Jambo na mkurugenzi wa Bonnah Kaluwa |
Akizungumza na Bloga hii mkurugenzi mtendaji wa Bonnah Education Trust Fund, na Diwani wa kata ya Kipawa jijini Dar Es salaam Mheshimiwa Bonnah Kaluwa alisema kuwa, uzinduzi huo umeambatana na maonyesho ya mavazi yaliyoanzia mnazi mmoja hadi mlimani City jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo ulipambwa michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi, maonyesho ya mavazi, pamoja na mabango mbalimbali yaliyokuwa na ujumbe wa elimu.
Washiriki katika maonyesho hayo wameelezea kufurahishwa kwao na kitendo cha Mheshimiwa Bonnah Kaluwa,kutambua umuhimu wa elimu katika familia masikini na kuamua kuwasaidia.
No comments:
Post a Comment